Kuhusu Elimuraia
Dhamira Yetu
Kwa sisi Elimuraia, elimu ni zaidi ya kuta za darasa na vitabu vya kiada. Tunakusudia kufanya upatikanaji wa fursa ya kujifunza kuwa rahisi, wezeshi, na sehemu ya maisha ya kila siku. Tumejitolea kuwapa Watanzania na wazungumzaji wote wa Kiswahili duniani jukwaa la kupata maarifa ya taaluma mbalimbali katika lugha ya Kiswahili kwa maendeleo yao binafsi na ya jamii kwa ujumla. Mbinu yetu ni kuandaa maudhui bora ya elimu ya kidijitali, ikijumuisha video, filamu na vitabu vya sauti (audiobooks). Bila shaka unapojifunza kwa lugha unayoielewa vizuri, unaweza kupata maarifa kwa ufanisi zaidi. Hivyo basi, jiunge nasi katika jitihada za ukuaji binafsi (personal growth) na kuendeleza jamii yetu kupitia elimu. Kumbuka, “kujua ni kuchagua.”
Maono Yetu
Maono yetu ni kuweka mazingira jumuishi na wezeshi ya kujifunzia ambayo yanasogeza maarifa karibu na wazungumzaji wote wa Kiswahili. Tunajitahidi kuwa jukwaa linaloongoza kwa maudhui ya elimu ya kidijitali katika Kiswahili, huku tukijenga daraja kati ya nchi zinazozungumza Kiswahili na nyinginezo duniani. Lengo letu ni kutoa uzoefu ng’amuishi na shirikishi wa kujifunza, kuwatia moyo watu wa rika zote wanaotaka kujifunza kudadisi uwezo wao na kujenga mazoea ya kujifunza wakati wote. Kwa maudhui yetu bora na mbinu za kipekee za utoaji elimu, Elimuraia imedhamiria kuleta mapinduzi ya jinsi wazungumzaji wa Kiswahili wanavyojifunza katika zama hizi za kidijitali. Hivyo, jiunge nasi katika safari hii ya urahisishaji wa upatikanaji wa maarifa.
Maadili yetu ya Msingi
- Upatikanaji: Tunajitahidi kufanya nyenzo za elimu zipatikane kwa Watanzania na wazungumzaji wote wa Kiswahili.
- Uwezeshaji: Tunaamini katika kuwawezesha wananchi kwa kuwapa maarifa na uelewa wa masuala ya kisiasa, kiuchumi na kijamii.
- Ushiriki: Tunalenga kujenga jamii ambayo wananchi wanashiriki kikamilifu katika kujielimisha.
- Ubora: Tunajitahidi kuandaa nyenzo za elimu zenye ubora na ufanisi katika kutoa maarifa.
- Heshima: Tunaheshimu haki ya mtu kujifunza na kupata elimu ili imsaidie kuweza kufikia uwezo wake kamili.
- Utofauti: Tunathamini mawazo, mtazamo na maoni tofauti.
- Ujumuishaji: Tunajitahidi kukuza mazingira jumuishi ambayo watu wenye historia na vipawa vya kila aina wanaweza kupata maarifa.
- Usawa: Tunaendeleza fursa za elimu zenye usawa kwa watu wote bila kujali asili au hali zao.
- Uadilifu: Tunajitahidi kudumisha viwango vya juu zaidi katika utendaji wa kazi yetu.
- Uwajibikaji: Tunajiwajibisha kwa ahadi na matendo yetu.
- Ushirikiano: Tunahimiza ushirikiano kati ya watu binafsi, mashirika na taasisi ili kuleta masuluhisho katika elimu yenye tija kwa Watanzania wote.
- Ubunifu: Tunajitahidi kupata mbinu bunifu katika ufundishaji na ujifunzaji ili wananchi waweze kufikia uwezo wao wa juu zaidi kifikra na kiutendaji.
- Uendelevu: Tunaamini katika kujenga uendelevu kupitia kazi yetu ili kufanya nyenzo za elimu zipatikane kwa vizazi hivi na vijavyo.
- Utu: Tunathamini utu wa watu wote na kutetea haki yao ya kuwa na maisha bora kupitia elimu.
Maoni mapya